Wananchi wa eneo la Tandale Mtaa wa Mkunduge |
JIJI la Dar es Salaam na vitongaji vyake, limekumbwa na maafa zaidi, mpaka jana vifo vya watu watano viliripotiwa, hali imebadirika usiku wa kuamkia leo na mpaka kufikia asubuhi ya leo vifo 13 vimesha ripotiwa ikiwemo vile vilivyosababishwa na radi na mshtuko, uharibifu wa miundombinu huku mamia ya watu wakikosa makazi, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazo endelea jijini Dar es laam kuanzia usiku wa kuamkia jumanne.Mvua hizo zimesababisha tatizo kubwa la usafiri kutokana na barabara kujaa maji, kuezua nyumba na kuua watu wapatao 13 mpaka sasa na kuacha maelfu ya wakazi wa jiji hilo bila makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na nyingine kuzama kabisa.
Mvua hizo zilianza kunyesha mnamo saa 9:00 alfajiri ya tarehe 21 zikiambatana na radi na ngurumo nzito na kusababisha kukatika mara kwa mara kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo ambalo ni kitovu kikuu cha biashara na uchumi kwa nchi.
Baadhi ya waokoaji wakiwa na vifaa vya kazi tayari kuokoa maisha ya wakazi wa mabondeni. |
Baadhi ya wakazi wakiwa sintofahamu baada ya kushuhudia mafuriko yaliochokuwa maisha ya wapendwa watatu. |
Mmoja ya wakazi akipima maji ili kuona uwezekano wa kwenda kuwasaidia watu waliozingirwa na maji. |
MH. RAISI PIA HAKUA NYUMA;
Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ameguswa na janga hilo na ametoa salam zake za rambirambi na pole kwa mkuu wa mkoa wa Dar es laam na wananchi wote waliofikwa na maafa hayo. Amefikisha ujumbe huo pia kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa facebook;
Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 vilivyotokana na mafuriko
yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar
es Salaam tokea juzi. Natuma rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili. Msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu a...See More
yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar
es Salaam tokea juzi. Natuma rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili. Msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu a...See More
No comments:
Post a Comment