Thursday, January 19, 2012

Nape akanusha kukivunja chama, akubali kuwepo makundi

* Asema kundi lake ni CCM


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,(CCM) Nape Nnauye.
 
Akiongea na Jambo Tanzania ya TBC1 Leo asubuhi, nnape nnauye amekanusha kuvunja chama kwa kauli zake , asema kama kutenganisha wachafu na wasafi ni kuvunja chama basi ni bora kikavunjika kwa mtindo huo, aidha, Nape amekubali kuwepo kwa makundi yanayo zalishwa na mpishano wa maadili na mgongan wa mawazo,jambo ambalo pia amelipiga vita.

“sheria nnazozisimamia zilikuwepo kabla sijazaliwa na ntakufa na kuziacha, hivyo basi kabla sijafa nimeapa kuzisimamia” Nape alitoa kauli hiyo  akisisitiza kua wale wachafu na walafi wasiopenda uwajibikaji ndio chanzo cha makundi, akiwafananisha na mtu mchafu anaekwenda kwenye kioo na kujiona mchafu na kukilaumu kioo badala ya kujitakasa, asema atabaki kua kioo akionesha wachafu kama walivyo hali kadharika wasafi na kwamba atasema ukweli hata kama utamgharimu.

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too