Sunday, July 24, 2011

Tanzania na siku ya mashujaa


by blogger, james mwamongi... monGi

Kila tarehe 25 mwezi wa saba ya kila mwaka watanzania huwa pamoja kuwakumbuka mashujaa(heroes) wote walio wahi kushiriki vita dhini ya utumwa na aina zote za kutawaliwa, ikiwa katika kawaida hiyo ya Watanzania,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu tarehe 25/07/2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa itaayofanyika kitaifa Naliendele, Mtwara.

Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Rais akiwa katika uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa Naliendele, atawaongoza viongozi wenzake kuweka silaha za asili katika mnara wa mashujaa.



Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Rais ataweka Mkuki na ngao, wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama ataweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini ataweka shada la maua, Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani ataweka upinde na mishale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion ataweka shoka.



Baada ya tukio hilo, kutakuwepo na sala kutoka kwa viongozi wa dini akiwemo Sheikh kwa niaba ya Waislam, Mchungaji kwa niaba ya C.C.T na Padre kwa niaba ya Roman Catholic.



Aidha gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama litatoa heshima kwa Mhe. Rais na kupiga wimbo wa Taifa kabla ya Rais Kikwete kutembelea makaburi na nyumba ya makumbusho ya Naliendele.



Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Tumkumbuke pia shujaa na Amiri jeshi mkuu na wakwanza, baba wa Taifa Mwalim j.k Nyerere ambaye pia alisherehekea siku hii, ifuatayo ni moja ya hotuba zake katika kuwakumbuka mashujaa wetu...

Mapambano Yanaendelea 1979

Ndugu Wananchi,
Leo ni siku ya Mashujaa. Siku hii kila mwaka tunawakumbuka mashujaa wetu waliojitoa kupigana na wavamizi kutoka katika nchi za nje au wageni waliotaka kuitawala nchi yetu. Tunawakumbuka, kwa heshima, wale walio-pigana kuwazuia Wakoloni wasiitawale Tanzania, na waie waliopigana katika vita vya Maji Maji katika jitihada za kupinga utawala wa Kijerumani.

Wachache wao tuna-wafahamu, na majina yao tunayaheshimu: mashujaa kama Mkwawa, Mirambo, na Mputa. Lakini wengi wao hatuwafahamu kwa majina; ila tunafahamu tu ya kwamba waiipigana, na kufa, katika jitihada za kutetea uhuru wa nchi yetu. Tunawakumbuka na kuwaheshimu.

Leo tena tunawakumbuka mashujaa hao kwa fahari. Juhudi zao na vitendo vyao vilitutia moyo siku za nyuma na vinatutia moyo mpaka sasa. Hatutawasahau.


No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too