Thursday, April 5, 2012

GODBLESS LEMA AENGULIWA NAFASI YAKE YA UBUNGE

Mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA, Godbless Lema

Kesi ya aliyekua mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema hatimae imesikilizwa tena leo ikiwa na mashauri nane yaliyochambuliwa na kumfanya jiji wa kesi hiyo kuhitimisha kwa kum-engua mheshimiwa huyo katika nafasi yake ya ubunge, na hivyo Mr. Godbless Lema si mbunge tena.

 Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na baadhi ya wanachama wa CCM wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, imefikia hatua hiyo baada ya kusubiliwa kwa muda sasa.

Akiongea na vyombo vya habri nje ya mahakama hiyo kasema hukumu hiyo ni Hasira Ya viongozi wa juu akimjumuisha Mh. Raisi, waziri mkuu na Mh. William Lukuvi.

Wakitoka mahakamani hapo wananchi waliomchagua mbunge huyo wameonyesha wa kukerwa na  kutoridhika na maamuzi hyo ya mahakama. wametoka kwa maandamano kuelekea katika ofisi za chama (CHADEMA) mkoani hapo na ndiko huko Mh. Godbless atatoa kauli yake pamoja na kauli ya chama, pia ataongea na wananchi na vyombo vya habari. Kwa yatakayo endelea kujili toka mkoani Arusha OTC itaendelea kukujuza...

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too