Saturday, April 7, 2012

STEVEN KANUMBA DIES

  • LULU KUHOJIWA
  • WATANZANIA WENGI ZAIDI WALIA 
 
Steven Kanumba the great enzi za uhai wake
Steven Kanumba the great, mfalme wa tasnia ya filamu Tanzania amefarikiki dunia. Habari hiyo yakusikitisha imeripotiwa kutokea saa sita usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa chanzo chetu wa habari tukio hilo limemhusisha Lulu ambaye pia ni msanii wa filamu na kwamba inawezekana wawili hao walikua na mahusiano ya kimapenzi hivyo tukio hilo limehusisha pia wivu wa mapenzi na usaliti, akiongea na mtandao huu mmoja wa ndugu wa karibu wa Kanumba ameeleza kua Kanumba amefariki na sababu ni yaweza kua presha, na kwamaba wakati wa tukio msanii huyo alikua na Lulu nyumbani kwake kinondoni, na simu ya lulu iliita akaenda kuipokea nje na kwasababu ya wivu wa kimapenzi alivorudi walianza majibishano wakiwa chumbani, huku sauti ya lulu akisikika kulia lakini baada ya muda Lulu alitoka akilia na kukimbia na walipoenda kumuangalia alikua amejilaza chini akiwa hana kovu ila povu kidogo hivyo kuhisi eidha alisukumwa au presha. Aidha swala hilo lipo chini ya vyombo vya usalama, na tutakufahamisha zaidi yatakayojili.

Wakiongea na vyombo vya habari wadau wa Tasnia na wapenzi wa msanii huyo wameonyesha kuguswa kwa kila hali.

Mtandao huu ukiungana na watanzania wote Tunamuombea Kanumba na Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu

KAZI ALIZOWAHI KUFANYA MAREHEMU

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too