Monday, April 2, 2012

YAMETIMIA, CHADEMA WACHUKUA JIMBO ARUMERU!

Joshua Nassari
Mgombea wa kiti cha ubunge Arumeru kupitia Chadema katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameibuka mshindi wa kura hizo.
Nassari ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu uliopita na marehemu Jeremiah Sumari, aliibuka kidedea katika kura hizo zilizopigwa jana katika jimbo hilo baada ya kujizolea kura 32,972 akifwatiwa na mpinzani wake mkuu kupitia CCM aliye jizolea kura 26,757.

Awali Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, alitamba kuwa chama hicho kitashinda katika uchaguzi huo kwa kuwa kina sera za kisanyansi zinazozingatia mambo yanayohitajika na wananchi. Alisema hakuna kulala mpaka kieleweke Arumeru na kusisitiza kuwa hata mafisadi wakimwaga fedha Chadema wanatumia mbinu ya kisanyansi zaidi kupata ushindi.
Kauli hizo zimepata baraka alfajiri ya leo kijana mdogo sumari alipotangazwa rasmi kuwa ndi mrithi wa Sumari, ambeye tunamuombea pumziko jema mbele ya haki.

 OTC tunamtakia kila la kheri na utekelezaji mwema wa ahadi alizoziweka wakati wa kampeni.

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too