Saturday, September 29, 2012

FRANCIS CHEKA KUVAANA NA NYILAWILA LEO, ATALINDA RECORD YAKE????

Francis cheka akipima uzito, Tayari kwa pambano lake badae.
Kalama Nyilawila akipima uzito, Tayari kwa pambano lake badae.
 

Manguli wa masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni leo Jumamosi kuonyeshana ubabe.
 

Cheka na Nyilawila wameshapigana mara tatu na katika mapambano yote Cheka aliibuka mshindi. Pambano la mwisho kwa manguli hao lilifanyika  morogoro ata hivyo lilizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambapo cheka aliibuka na ushindi wa point.

Pambano la leo litafanyika katika ukumbi wa PTO uliopo viwanja vya sabasaba jijini Dar es laam.

Mpaka sasa record ya cheka ni kwamba amepigana mechi 40, na kati ya hizo kashinda 32, droo 2 na kupigwa mapambano 6, wakati mpinzani wake amepigana mechi 26, kapigwa 4 na droo 2.

Kaa nasi kwa matokeo ya mechi hiyo hapo baadae....

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too