Tuesday, September 18, 2012

MARIAH CAREY AKANUSHA TETESI ZA KUWA NA BIFU NA Nicki Minaj

Randy Jackson, Mariah Carey, Ryan Seacrest, Nicki Minaj, and Keith Urban

Ikiwa ni siku mbili tu ndani ya auditions kwa ajili ya msimu mpya wa "American Idol," tayari kuna fununu kwamba Mwanadada Mariah Carey na jaji mwenzake -Nicki Minaj wana bifu la chinichini. Lakini diva wa pop Mariah carey amekanusha uvumi huo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu.

"Je ni vipi tunaweza kutengeneza bifu ndani ya siku mbili? Hata kama lipo acheni lichukuchukue muda mrefu kidogo kuenea basi, "alitania mwanadada huyo(Mariah) aliyekuwa ameketi kando ya nyota country music Keith Urban na Nicki katika meza ya majaji '.

"Ni furaha. Ni muziki. Ni kuimba. Ni vicheko, "aliongeza kama sababu za kwanini wawe na bifu mapema hivyo.

Mariah na Nicki walishirikiana kwenye remix ya single ya
Mariah 2010 “Up Out My Face.”

No comments:

Post a Comment

Infolinks In Text Ads

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

we gOt friends too